Mabomu mawili yaliyotegwa katika magari yakilenga vituo vya usalama katika mji wa Aleppo yameuwa kiasi watu 28, huku waasi wakiishutumu serikali ya nchi hiyo kwa kuanzisha mashambulizi ili kuepuka lawama.
Mgomo wa madaktari nchini Tanzania, ambao umedumu kwa zaidi ya wiki mbili sasa hatimae umemalizika na madaktari hao kuanza kazi huku Madaktari hao wakihimiza serikali kutekeleza madao yao ya msingi.
Huenda visa vya kigaidi vikaongezeka duniani kufuatia kundi la Al Qaeda kutangaza wazi kwamba kundi la waasi nchini Somalia Al shabaab limejiunga rasmi na wanamgambo hao wa kigaidi.
Mataifa ya eneo la euro yanataka kuendelea kutoa msaada kwa Ugiriki lakini kwanza ni pale tu nchi hiyo ambayo imezongwa na madeni itakapopiga hatua ya kutimiza masharti yote yanayotakiwa na Umoja wa Mataifa ya Euro.
Watu 31 wameuwawa Syria baada ya vikosi vya Jeshi la Rais Bashar al- Assad kuushambulia mji wa Homs, huku Israel ikionya juu ya uwezekano wa silaha za Syria kupelekwa kwa kundi la Hizbullah la Lebanon.
Mahakama ya Maldives imetoa waranti wa kuwezesha kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa visiwa hivyo, Mohammed Nasheed, pamoja na aliyekuwa waziri wake wa ulinzi huku jeshi likitumwa katika mji wenye machafuko wa Addu.
Mazungumzo ya wanasiasa nchini Ugiriki yamemalizika bila muafaka juu ya mageuzi na hatua za kubana matumizi, ambavyo viliwekwa na wakopeshaji kama sharti la kupewa mkopo mpya wa kuinusuru nchi hiyo usifirisike.
Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa
Ni shida kwa mwanaadamu anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio ya kawaida, kuamini kwamba anaweza mara moja kujikuta akiwa ameanguka chini akiwa amepoteza kila kitu maishani, akiwa katikati ya mateso na idhilali.
Tembelea DW katika Facebook
Tembelea DW katika Twitter
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.