1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages


 

Matukio ya Kisiasa | 16.05.2008

Ziara ya Kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama Ujerumani

Mivutano baina ya wanasiasa wa vyama vinavyounda katika serikali kuu mjini Berlin kuhusu ziara hiyo

Kiongozi wa kiroho wa Tibet aliwasili jana kwa ziara ya siku tano  Dalai Lama  nchini  Ujerumani, akisisitiza kwamba utamaduni wa mchanganyiko wa Tibet pamoja na maadili yake ya utajiri mkubwa  katika dini ya Buddha, ni mambo yanayosisitiza umuhimu wa  kuwepo kwa utawala wa kweli wa ndani kuweza kujiamulia mambo yake yenyewe ya ndani ya China ilio moja.

Katika ziara hii Dalai Lama  amepangiwa mikutano  na wanasiasa kadhaa akipanga pia kutoa mihadhara minne kabla ya  hotuba yake ya mwisho Jumatatu ijayo kwenye lango la Brandenburg mjini Berlin. Aidha mshindi huyo wa  tunzo ya amani ya Nobeli 1989,amesha onana  na  Mawaziri wakuu wawili wa mikoa kutoka chama cha Christian Democrats CDU cha Kansela Angela Merkel  ambao ni Juergen Ruettgers wa North Rhine-Westphalia na Rolandt Koch wa mkoa wa Hesse, pamoja na  Spika wa bunge la Ujerumani Norbert Lammert.

Wakati akiwasili  kiongozi huyo wa kidini wa Tibet alisisitiza kwamba anachopigania na  malaka  ya utawala wa kweli wa ndani  wa Tibet na kusema hilo halinabudi kufikiwa bila matumizi ya nguvu. Akaongeza  kwamba  Tibet na China zina urithi wa pamoja wa utamaduni na mambo mengine, akiongeza kwamba anachopigania zaidi ni heshima ya binaadamu.

Lakini ziara yake hapa Ujerumani kwa upande mwengine imezusha mivutano miongoni mwa wanasiasa  ndani ya serikali ya mseto baina ya CDU na Wasocial democrats SPD. Waziri mkuu wa mkoa wa  Hesse Ronald Koch amemkosoa tena waziri wa mambo ya nchi za nje  Frank-Walter Steinmeier kutoka chama cha SPD kwa  uamuzi wa kutokutana na  Dalai Lama wakati wa ziara hii. Akizungumza katika  toleo la leo la gazeti la" Neuen Presse", Bw Koch alisema hatua hiyo inaashiria kutoeleweka kwa  sera ya serikali ya Ujerumani kuhusiana na haki za binaadamu.

Wakati huo huo akapongeza  mkutano unaopangwa kufanyika Jumatatu kati ya Dalai Lama na Waziri wa misaada ya maendeleo Bibi Heidemarie Wieczoek-Zeul akisema uamuzi wa mwanasaiasa huyo wa SPD ni wa kijasiri.

Dalai Lama hatokutana pia na  Kansela Merkel ambaye kwa wakati huu yuko  mjini Lima -Peru akihudhuria mkutano  mkuu wa Viongozi wa Amerika kusini na  nchi za Umoja wa Ulaya unaoanza leo.

Baadhi ya wanasiasa  na wadadisi wameikosoa sera ya serikali ya Ujerumani kuelekea China, wakisema inaligubika suala la  ukiukaji wa haki za binaadamu na kutoa kipa umbele kwa masilahi ya  kiuchumi kwa sababu ya umuhimu wa China kibiashara. Ubalozi wa China mjini  Berlin umetoa taarifa ukilalamika juu ya  mkutano huo kati ya  Bibi Wieczorek-Zeul na Dalai Lama.

Taarifa ya ubalozi huo imesema  pamoja na kwamba China inataka kuzungumza na Ujerumani  kuhusu Tibet lakini ni lazima sera ya China ilio moja  izingatiwe na  kuimarishwa. Mkutano kama huo mwaka jana   baina ya Kiongozi huyo wa kidini wa Tibet na Kansela Merkel ulizusaha msuko suko kidogo katika uhusiano kati ya Berlin na Beijing.

Leo Dalai Lama amepangiwa kutoa mhadhara katika kituo cha mikutano mjini Bochum juu ya haki za binaadamu na utanda wazi.

 

Abdulrahman, Mohamed

 
Share this article

Send us an e-mailSendPrint

More on the topic



 
Picture of the Day
ImageOfTheDay

DW-TV EUROPE live

Journal (deutsch) - Mit Reporter