Ufunguzi rasmi wa kituo maalum cha kupata maelezo kuhusu matangazo ya DW unafanyika leo katika taasisi ya mafunzo ya lugha ya Kijerumani ya Goethe jijini Dar es salaam.
Nembo ya Goethe Institut
Nembo ya Shirika la Ujerumani la huduma za maendeleo
Baada ya ufunguzi huo, Shirika la utangazaji la kimataifa la Ujerumani Deutsche Welle pamoja na taasisi ya DED/INWENT itaendesha mdahalo, kuhusu mchango wa vyombo vya habari kuelekea katika uchaguzi mkuu baadae mwaka huu nchini Tanzania.
Nembo ya shirika la INWENT
Mdahalo huo utaongozwa na Mhariri Mkuu wa DW, Marc Koch, mkuu wa idara ya matangazo ya lugha za Kiafrika na Mashariki ya Kati ya DW, Ute Schaeffer na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt.
Mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, George Njogopa ametutumia taarifa ifuatayo:
Mtayarishaji: Samia Othman
Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed