| 16.05.2008 | 15:00 UTC
Bush - Israel yaweza kuitegemea Marekani.
Jerusalem.
Rais Bush wa Marekani ameliambia bunge la Israel kuwa Marekani itasimama pamoja na Israel katika kuipinga Iran iwapo itajaribu kujipatia silaha za kinuklia.
Bush ameongeza kuwa anakichukulia kwa umuhimu wa juu kitisho kilichotolewa na rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad kuifuta Israel kutoka katika ramani ya dunia. Akizungumza umuhimu wa kuitetea Israel katika mashariki ya kati Bush amesema.
O-Ton Bush
Iran imesema kuwa mpango wake wa kinuklia una lenga katika matumizi ya umeme.
Bush, ambaye yuko katika ziara kuadhimisha kuasisiwa kwa taifa la Israel miaka 60 iliyopita, ameliambia bunge la Israel , Knesset kuwa Israel pia inaweza kutegemea uhusiano usiolegalega na Marekani.
Rais Bush ameondoka nchini Israel alielekea nchini Saudi Arabia leo kuanza ziara nchini humo , ambayo itakuwa ni maadhimisho ya miaka 75 ya uhusiano baina ya Marekani na nchi hiyo ya Kifalme.






