| 16.05.2008 | 15:00 UTC
Bin Laden awashutumu viongozi wa mataifa ya magharibi kuhusu miaka 60 ya Israel
Dubai.
Kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda Osama bin Laden amewashambulia viongozi wa mataifa ya magharibi kwa kushiriki katika maadhimisho ya miaka 60 ya kuasisiwa kwa taifa hilo la Kiyahudi.
Akizungumza katika ujumbe wa katika radio leo Ijumaa , bin Laden ameapa kuendeleza mapambano dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi pamoja na washirika wake na kwamba Waislamu hawatasalim amri hadi pale Palestina itakapokombolewa kabisa.
Ujumbe huo leo umekuja wakati rais wa Marekani George W. Bush anakamilisha ziara yake nchini Israel kuadhimisha miaka 60 tangu kuasisiwa kwa taifa hilo.
Bin Laden amesema katika ujumbe huo kuwa mapambano kwa ajili ya Palestina ni jambo linalosukuma vita vya Al-Qaeda dhidi ya mataifa ya magharibi.






