| 16.05.2008 | 15:00 UTC
Rais wa China aenda katika eneo la tetemeko.
Beijing.
Rais wa China Hu Jintao amekwenda katika mji wa Mianyang katika jimbo la Sichuan kuona binafsi maafa yaliyotokea siku ya Jumamosi baada ya tetemeko la ardhi kutokea katika eneo hilo.
Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuwa rais Hu ametoa wito wa kuongezwa juhudi katika kile alichokieleza kuwa ni awamu muhimu ya operesheni ya uokozi.
Maafisa sasa wanasema , wanahofu kuwa idadi ya watu waliokufa inaweza kuwa juu zaidi ya 50,000.
Hadi sasa , kiasi cha watu 22,000 wamethibitishwa kuwa wamefariki, lakini watu wengine kwa maelfu hawajulikani waliko. Mji wa Mianyang umekuwa kituo cha kupokea watu walionusurika wanaomiminika kutoka katika maeneo yaliyoathirika karibu na eneo tetemeko hilo lilipotokea kilometa 100 upande wa magharibi.






