| 16.05.2008 | 15:00 UTC
Mzozo wa Chavez na Merkel wagubika mkutano wa L.America.
Lima.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi msaada kutoka Ujerumani kwa ajili ya wizara ya mazingira nchini Peru wakati wa mkutano na rais wa nchi hiyo, Alan Garcia.
Kufuatia mazungumzo ya viongozi hao wawili, Garcia ameeleza kumuunga kwake mkono Merkel katika mvutano wake wa hivi karibuni na rais wa Venezuela Hugo Chavez.
Merkel anatarajiwa kukutana na Chavez , kandoni mwa mkutano wa umoja wa Ulaya na mataifa ya Latin Amerika unaofanyika leo Ijumaa katika mji mkuu wa Peru , Lima.
Mkutano huo unatarajiwa kujadili umasikini na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini umegubikwa na mzozo kati ya viongozi hao wa Ujerumani na Venezuela. Merkel amezitaka nchi za eneo hilo kujiweka mbali na serikali ya kisishalist ya Venezuela, wakati Chavez amemshutumu Merkel kwa kuwa katika utamaduni ule ule wa kisiasa wa enzi za Nazi.






