| 16.05.2008 | 15:00 UTC
dalai Lama atoa wito wa kujitawala zaidi Tibet
Bochum, Ujerumani.
Kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai lama anaendelea na ziara yake ya siku tano nchini Ujerumani akiwa katika mji wa Bochum.
Kiongozi huyo wa kidini amewashukuru waungaji wake mkono katika bara la Ulaya wakati kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa anatafuta kujitawala zaidi kwa jimbo lake la Tibet, na sio uhuru kamili.
Jana Alhamis Dalai Lama alikutana na viongozi wa kisiasa wa eneo la Ulaya pamoja na rais wa bunge la Ujerumani, Nobert Lammert.
China tayari imepinga mipango ya kukutana siku ya Jumatatu na waziri wa maendeleo wa Ujerumani Heidemarie Wieczorek-Zeul.
Mwaka jana kansela Angela Merkel alikutana na Dalai Lama mjini Berlin, hatua ambayo ilisababisha uhusiano kati ya China na Ujerumani kuingia dosari.






