| 08.07.2008 | 15:00 UTC
Mazungumzo ya nyuklia ya Korea Kaskazini kuanza tena
Beijing
China imesema mazungumzo na pande sita kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini yataanza tena wiki hii kwa mara ya kwanza kwa muda wa miezi 9. Mazungumzo hayo ambayo yamepangwa kufanyika tarehe 10 mwezi huu, yanafanyika baada ya Korea ya Kaskazini kuikabidhi Uchina hati ya tathmini ya shughuli zake za nyuklia na kuteketeza kinu chake muhimu cha kurutubisha madini ya uranium mwezi uliopita.
Nchi zinazohusika na mazungumzo hayo ni pamoja na China, Japan, Urusi, Marekani na Korea Kaskazini na Kusini. Wajumbe watazungumzia juu ya hatua nyingine zinazotakiwa katika utaratibu mzima wa kukomesha shughuli za kinyuklia za Korea ya kaskazini.





