1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages



 

 | 08.07.2008 | 15:00 UTC

Waziri wa fedha wa Kenya aomba kujiondoa barazani

Nairobi


Waziri wa fedha wa Kenya, Amos Kimunya, ameomba kujiondoa katika baraza la mawaziri ili kuupisha uchunguzi kutokana na kashfa ya rushwa inayomuandama kufuatia kuuzwa kwa hoteli ya kifahari ya Grand Regency.Hoteli hiyo iliuzwa kwa wawekezaji  wa Libya. Ripoti ya mwanasheria mkuu wa Kenya Amos Wako ilipendekeza Bwana Kimunya wa chama cha PNU kujiondoa serikalini wakati uchunguzi unaendelea. Wiki iliyopita bunge la Kenya lilipiga kura ya kutokuwa imani na utendaji wake katika suala hilo.Hata hivyo Bwana Kimunya anashikilia kuwa hana hatia.

.

Benki kuu nchini Kenya iliuza hoteli ya Grand Regency kwa bilioni 2.1 shillings za Kenya sawa na milioni 44.4 za dola za kimarekani lakini wabunge wanadai kuwa thamani yake halisi ilikuwa karibu bilioni 7 za shillings za Kenya.


Suala hilo ndilo tatizo la hivi karibuni kabisa kwa serikali ya mseto ya Kenya. Waziri wa ardhi,James Orengo, kutoka chama cha waziri mkuu Raila Odinga cha ODM amesema anataka kuomba mkataba wa mauzo hayo ubatilishwe na sheria.