1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages



 

 | 08.07.2008 | 15:00 UTC

Marekani na jamhuri ya Czech zasaini mkataba wa makombora ya ulinzi

Prague


Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleeza Rice amesaini  mkataba wa makombora ya kujihami na mwenzi wake wa Jamhuri ya Czech Karel Schwarzenberg katika mji mkuu wa nchi hiyo Prague hii leo. Mkataba huo unairuhusu Marekani kujenga na kuendesha kituo cha rada karibu na mji mkuu Prague kama sehemu ya mfumo wake wa makombora ya ulinzi. Mpango huo unapingwa na raia wa Czech na huenda serikali ya mrengo wa kulia na kati ukahitaji kura kutoka upinzani ili iweze kuidhinisha mkataba huo.


Marekani imo mbioni kufikia mkataba na Poland pia kuweka idadi fulani ya vituo vya kunasa makombora. Serikali ya Poland imekuwa ikiomba misaada zaidi ya kijeshi kutoka kwa Marekani na pande hizo mbili zinasema ziko karibu kufikia makubaliano. Marekani inasema ulinzi huo unanuia kuzuwia mashambulizi kutoka nchi ambazo ni kitisho kwao  kwa mfano Iran.

Urusi inapinga mpango mzima wa kutengeza makombora ya kujihami  ambao inauzingatia kama kitisho.