DW-WORLD.DEPrint

16.05.2008

Mkutano wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali duniani wafanyika mjini Belfast,Ireland

Mwenyekiti wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba yuko Belfast,Ireland Kaskazini

Huko mjini Belfast Ireland ya Kaskazini, kunafanyika mkutano wa Umoja wa Vyama Vya Kiliberali duniani, ambapo wajumbe kutoka takriban vyama 100 kutoka sehemu mbalimbali duniani wanahudhuria.

Miongoni mwao ni Rais Abdulaye Wade wa Senegal, Morgan Tsvangirai kutoka chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe na Profesa Ibrahim Lipumba mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, ambaye alizungumza na Aboubakary Liongo, kwanza akielezea madhumuni ya mkutano huo.

DW-WORLD.DEPrint

| www.dw-world.de | © Deutsche Welle.